Wednesday, June 1, 2011

UPAMBAJI WA HARUSI

Upambaji wa harusi wa kisasa mwingi hutumia maua na rangi mahsusi za harusi tofauti na zamani ambako tulikuwa tunaujaza ukumbi mwa mapulizo ya rangi tofauti

Zaidi ya maua ridi 'roses' pia kuna nakshi nakshi nyenginezo ambazo hutumika ikiwa ni vitambaa vya hariri nataa za rangi ya sherehe.

Mbali na hayo siku hizi pia kuna mapamba special ambayo hayaitaji kuweka kitambaa wala yale makopo ya maua kama msitu ambao mie nahisigi muda wowote anafumuka nyoka kama si kuangukiwa na kinyonga, yenyewe husimama kama background tu.

Na kwa sasa si kwamba tunapamba kwa bwana na bibi harusi pekee yaani pale mbele, la hasha siku hizi hadi kwa waalikwa hupambwa kila meza hutandikwa kitambaa na viti vikavishwa vitambaa na kunakshwa na tai kuuubwa ya rangi ya harusi

No comments:

Post a Comment